Lugha Nyingine
Msanii wa Ethiopia abuni sanaa kutokana na ufunuo wa ?kitabu maarufu cha China “Yi Jing” (3)
Msanii Dawit Muluneh akichora picha ya neno la Kichina katika Jumba la Uchoraji wa Picha lililopo Addis Ababa, Ethiopia tarehe 18, Machi, 2024. (Xinhua/Michael Tewelde) |
Katika Jumba la Uchoraji wa Picha lililoko kiini cha Addis Ababa, Ethiopia, msanii Dawit Muluneh mwenye umri wa miaka 50 akisimama mbele ya turubai, anachora kwa makini picha ya neno la Kichina la zama za kale.
Pembeni yake ni sanaa za picha zilizochorwa naye kutokana ufunuo wa kitabu maarufu cha China “I Ching” (katika lugha ya Kichina "Yi Jing"), kitabu ambacho kimejulikana kwa zaidi ya miaka 2,000 na kingali bado ni moja kati ya vyanzo vya utamaduni wa China.
Msanii huyo amechora picha 64 , ambazo zinawakilisha alama 64 katika kitabu cha “Yi Jing” cha China, alama hizo zinaonesha mawasiliano ya kila siku kati ya binadamu na mazingira ya asili. Kwenye picha hizo kuna maelezo yaliyoandikwa kwa lugha ya Kichina, Kiingereza na Kiamhari yanayowaelezea watazamaji ujuzi na hisia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma