Lugha Nyingine
Kampuni binafsi katika Mkoa?wa Fujian wa China zashuhudia ukuaji wa biashara ya nje katika miezi miwili ya kwanza ya 2024 (3)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 22, 2024
Wafanyakazi wakifanya kazi kwenye kiwanda cha Kampuni ya Teknolojia ya Contemporary Nebula huko Fuzhou, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China, Machi 20, 2024. (Xinhua/Lin Shanchuan) |
FUZHOU - Katika miaka ya hivi karibuni, kampuni binafsi katika Mkoa wa Fujian, China zimekuwa zikijikita katika mahitaji mapya ya soko la kimataifa, zikiongeza uvumbuzi wa Teknolojia na kupanua masoko ya ng'ambo na njia za mauzo. Takwimu kutoka idara ya forodha zinaonyesha kuwa kuanzia Januari hadi Februari mwaka huu, thamani ya biashara ya kuagiza na kuuza bidhaa nje ya nchi ya kampuni hizo binafsi katika mkoa huo ilifikia yuan bilioni 207.35 (kama dola za Marekani bilioni 28.79), ikiwa ni ongezeko la asilimia 21.9 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma