Lugha Nyingine
Mkoa wa Fujian washuhudia mkupuo mkubwa zaidi wa usafirishaji wa magari nje
Magari elfu nne yaliyoundwa na karakana ya magari ya abiria ya kiwanda cha Ningde cha Kampuni ya Magari ya SAIC yamepakiwa kwenye meli ya kubeba magari ya "Wisdom Ace" siku ya Jumanne kwenye Gati la Jiangyin la Bandari ya Fuzhou, Mkoa wa Fujian, Kusini Mashariki mwa China. Shehena hiyo ya magari itasafirishwa katika nchi mbalimbali zikiwemo Uholanzi, Misri na Uingereza. Kwa mujibu wa ripoti, huu ni mkupuo mkubwa zaidi wa usafirishaji wa magari nje ya nchi kwa Mkoa wa Fujian, ambao unajumuisha magari yanayotumia nishati mpya 2,800.
Takwimu za forodha zinaonyesha kuwa kuanzia Januari hadi Februari mwaka huu, Mkoa wa Fujian umesafirisha nje ya nchi magari 15,377 yenye thamani ya yuan bilioni 2.07 (kama dola za Kimarekani milioni 288.41), ikiwa ni ongezeko la asilimia 123 na asilimia 69 mtawalia ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma