Lugha Nyingine
Uchimbaji wa kisima cha aina yake chenye kina kirefu zaidi chini ardhini cha China wazidi mita 10,000
URUMQI - Uchimbaji wa kisima chenye kina kirefu zaidi katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, Kaskazini Magharibi mwa China umefikia mita 10,000 siku ya Jumatatu, majira ya saa 8:48 mchana (kwa saa za Beijing) na bado unaendelea kwenda kwenye kina cha chini zaidi, ikiashiria mafanikio ya China katika utafiti wa kina wa Dunia.
Kikiwa kinapatikana katika sehemu ya pembezoni mwa Jangwa la Taklimakan katika Bonde la Tarim, Kisima hicho cha "Shenditake 1" kinatarajiwa kufikia kina kilichopangwa cha mita 11,100 baada ya kukamilika. Ni kisima cha kwanza cha utafiti wa kisayansi nchini China kilichofikia kina cha zaidi ya mita 10,000.
Tangu kuanza kwa uchimbaji wake Mei 30, 2023, kisima hicho kimepenya matabaka 13 ya bara, na mabomba zaidi ya 1,000 ya kuchimba visima yakiendeshwa kupenya ardhini kwenye Dunia huku vifaa 20 vya kuchimbua ardhini vikiwa zimetumika katika mchakato huo.
"Ni mara ya kwanza kwa China kuchimba kisima chenye kina kirefu cha mita zaidi ya 10,000 kwenda chini," amesema Wang Chunsheng, mtaalam mkuu wa Kampuni ya Tarim Oilfield ya Shirika la Petroli la China, ambayo inasimamia uchimbaji huo.
Likiwa linapatikana kati ya milima ya Tianshan na Kunlun, Bonde la Tarim ni mojawapo ya maeneo magumu sana kwa kufanya utafiti kutokana na mazingira yake magumu ya ardhini na hali ngumu ya chini ya ardhi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma