Lugha Nyingine
Magari zinazotumia nishati ya umeme za kampuni za China zaonekana kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Magari ya Geneva (3)
Picha iliyopigwa tarehe 28, Februari ikionesha banda la BYD katika Maonesho ya 91 ya kimataifa ya Magari ya Geneva, Switzerland. (Xinhua) |
Maonesho ya 91 ya kimataifa ya Magari ya Geneva tarehe 27 Februari yalifunguliwa rasmi kwa umma na yataendelea hadi tarehe 3, Machi.
Maonesho ya kimataifa ya Magari ya Geneva yaliyoanzia mwaka 1924 siku zote yanajulikana kama alama ya mwelekeo wa viwanda vya magari. Kaulimbiu ya Maonesho ya mwaka huu ni “Magari ya Hivi Leo na Baadaye” , na yamevutia makumi ya kampuni za magari kushiriki. Kampuni za China zimeleta magari ya aina mbalimbali yanayotumia nishati ya umeme kwenye maonesho hayo, ambayo yamefuatiliwa na watu wengi.
Katika mabanda ya magari ya China, watazamaji wengi wamekuja kutembelea. Kwenye banda la Shirika la Magari la Shanghai (SAIC MOTOR), magari kumi yanayotumia nishati ya umeme yameonekana pamoja, yakiwemo magari ya IM L6 na MG3 HEV yaliyooneshwa kwa mara ya kwanza. Kampuni ya BYD pia imeleta magari tisa yanayotumia nishati ya umeme kwenye maonesho hayo.
Katika magari ya aina 20 yaliyooneshwa kwenye mkutano na waandishi wa habari wa tarehe 26, mengi zaidi yanatumia nishati mpya, na miongoni mwao magari yanayotumia umeme tu yalichukua zaidi ya nusu, hali ambayo imeonesha mwelekeo wa viwanda vya magari vya dunia nzima vya kuendeleza magari ya kutumia nishati ya umeme.
Daraja la kuvuka Mto Yangtze la Longtan likiendelea kujengwa huko Nanjing, China
Watawa 12 wapata shahada yenye hadhi sawa na uzamivu katika Ubuddha wa Tibet, China
Sherehe kwenye hekalu zafanyika Mkoa wa Henan katikati ya China
Boti nyingi zafanya safari baharini katika Mji wa Sanya, Mkoani Hainan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma