Lugha Nyingine
Kampuni yanufaika kutokana na maendeleo yaliyoratibiwa ya Beijing-Tianjin-Hebei
Jingwei Hirain ni kampuni inayoongoza katika Nyanja ya mifumo ya kielektroniki ya magari yenye makao yake makuu mjini Beijing, China. Mwaka 2016, kampuni hiyo ilihamishia kiwanda chake cha uzalishaji hadi Tianjin na kupata maendeleo ya haraka, ikitumia fursa ya maendeleo yaliyoratibiwa ya Beijing-Tianjin-Hebei.
Mamlaka za serikali za mitaa huko Xiqing zimefanya juhudi za kujenga mazingira mazuri ya biashara kwa kampuni, kutoa usaidizi mbalimbali kama vile kuboresha michakato ya uidhinishaji, kuanzisha mifumo ya mawasiliano ya mara kwa mara, na kupunguza gharama za kupanga ofisi kwenye majengo ili kutoa usaidizi thabiti kwa kampuni.
Julai 2023, Kituo cha Utafiti na Uendelezaji wa Bidhaa (R&D) cha Jingwei Hirain, chenye uwekezaji wenye thamani ya jumla ya yuan bilioni 1.679 (kama dola za Kimarekani milioni 233.2), kilianza kufanya kazi. Kwa sasa kina wafanyakazi zaidi ya 1,600 wa utafiti na uendelezaji bidhaa. Msingi mpya wa uzalishaji wa kampuni hiyo, wenye uwekezaji wa thamani ya jumla ya yuan takriban bilioni 1 (kama dola za Kimarekani milioni 138.9), pia unajengwa huko Tianjin kwa mujibu wa viwango vya karakana za teknolojia za akili mnemba.
Hivi sasa, Kampuni ya Jingwei Hirain imeanzisha ujenzi wa kipindi cha pili wa Kituo cha Utafiti na Uendelezaji Bidhaa (R&D) cha Tianjin katika Eneo la Xiqing ili kuchangia kuongeza kasi ya uundaji wa nguvu mpya za uzalishaji.?
Sherehe kwenye hekalu zafanyika Mkoa wa Henan katikati ya China
Boti nyingi zafanya safari baharini katika Mji wa Sanya, Mkoani Hainan, China
Sherehe ya "Kuonyesha Buddha" yafanyika katika Hekalu Kaskazini Magharibi mwa China
Watu wa kabila la Wagelao washerehekea Sikukuu ya Maolong huko Guizhou, Kusini Magharibi mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma