Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping afanya mazungumzo na Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio (5)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amefanya mazungumzo Jumatano mjini Beijing na Rais wa Jamhuri ya Sierra Leone Julius Maada Bio, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, ambapo ameeleza kuwa China na Sierra Leone zinafurahia urafiki uliotukuka wa muda mrefu na zimekuwa zikiungana mkono katika masuala yanayohusu masilahi yao ya msingi na yanayofuatiliwa na pande zote, zimefanya ushirikiano mzuri katika nyanja mbalimbali za maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Uhusiano kati ya China na Sierra Leone ni mfano mzuri wa mshikamano na ushirikiano kati ya China na Afrika, Rais Xi amesema, na kuongeza kuwa China inapenda kujiunga na Sierra Leone katika kuimarisha hali ya kiwango cha juu ya kuaminiana kisiasa, kuendeleza ushirikiano wa matokeo halisi na wa kunufaishana, na kuimarisha uratibu katika masuala ya kimataifa na kikanda, na kusukuma uhusiano wa pande mbili katika ngazi mpya.
Rais Xi amesema China inaunga mkono kithabiti watu wa Sierra Leone katika kufuata njia ya maendeleo inayoendana na hali halisi ya nchi yao. Amesema China ingependa kuimarisha hali ya kubadilishana mawazo na Sierra Leone kuhusu utawala wa nchi, na kuendelea kuungana mkono na Sierra Leone katika masuala yanayofuatiliwa na kila upande na kulinda mamlaka ya nchi, usalama na maslahi ya maendeleo.
China pia ingependa kutoa usaidizi na uungaji mkono kwa kadiri iwezavyo kwa maendeleo ya Sierra Leone katika kilimo, ujenzi wa miundombinu na rasilimali watu , na kuhimiza kampuni za China kuwekeza na kufanya biashara nchini Sierra Leone, Rais Xi amesema.
Rais wa China ameikaribisha Sierra Leone kushiriki katika Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia, na kuendeleza kwa pamoja ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
Amesema, China ingependa kufanya juhudi pamoja na marafiki wa Afrika, ikiwa pamoja na Sierra Leone, kufanikisha mkutano wa mwaka huu cha Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).
Rais Julius Maada Bio amesema China ni rafiki wa kuaminika na wa kutegemewa, akiishukuru China kwa uungaji mkono wake mkubwa kwa maendeleo ya Sierra Leone katika uchumi na jamii.
Amezungumzia sana juu ya Chama cha Kikomunisti cha China kuongoza watu wa China kufikia maendeleo makubwa na kuhimiza ustawishaji wa taifa. Bio amesema uzoefu wa China unatoa msukumo kwa nchi zinazoendelea kuharakisha maendeleo yao.
Sherehe kwenye hekalu zafanyika Mkoa wa Henan katikati ya China
Boti nyingi zafanya safari baharini katika Mji wa Sanya, Mkoani Hainan, China
Sherehe ya "Kuonyesha Buddha" yafanyika katika Hekalu Kaskazini Magharibi mwa China
Watu wa kabila la Wagelao washerehekea Sikukuu ya Maolong huko Guizhou, Kusini Magharibi mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma