Lugha Nyingine
China yaanza ujenzi wa awamu ya 2 ya mradi wa nishati ya nyuklia wa Zhangzhou (2)
Picha iliyopigwa Februari 22, 2024 ikionyesha ujenzi wa kipindi cha pili wa mradi wa nishati ya nyuklia katika mji wa Zhangzhou Mkoa wa Fujian, Kusini Mashariki mwa China. (Xinhua) |
BEIJING - China imeanza ujenzi wa kipindi cha pili cha mradi wa nishati ya nyuklia katika Mji wa Zhangzhou wa Mkoa wa Fujiang kwa kutumia vinu vya nyuklia vya Hualong One, ambavyo ni vinu vya kizazi cha tatu vilivyotengenezwa kwa kujitegemea nchini China.
Shirika la Taifa la Nyuklia la China limeseam, kundi la kwanza la mashine nne la Hualong One limeshakamilika na kuanza kutumika.
Mradi huo wa nishati ya nyuklia wa Zhangzhou umesanifiwa kujumuisha mashine sita za nishati ya nyuklia, kila mashine ina uwezo wa kuzalisha umeme wenye nguvu za kilowati milioni 1.
Vinu vya nyuklia vya Hualong One viliundwa na kampuni kubwa mbili za nishati ya nyuklia: Kundi la Kampuni za Nishati ya Nyuklia za China na CNNC.
Kwa mujibu wa CNNC, kila mashine ya nishati ya nyuklia ya Hualong One ina uwezo wa kuzalisha kilowati za umeme zaidi ya bilioni 10 kwa saa kwa mwaka, ambazo zinaweza kukidhi mahitaji ya kila mwaka ya uzalishaji na mahitaji ya umeme ya nchini ya watu milioni 1 katika nchi zilizoendelea kwa wastani.
Watu wa kabila la Wagelao washerehekea Sikukuu ya Maolong huko Guizhou, Kusini Magharibi mwa China
Wakulima kote China wawa na pilika nyingi za uzalishaji wa kilimo wakati Siku ya Yushui yakiwadia
Ndege C919 ya China yashiriki mazoezi ya Maonyesho ya Anga ya Singapore
Chuo Kikuu cha Kenyatta chafanya maonyesho ya dragoni wa China ili kukuza mawasiliano ya kitamaduni
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma