Lugha Nyingine
Ndege ya abiria ya C919 ya China yashiriki kwa mara ya kwanza kwenye Maonyesho ya Ndege ya Singapore
Ndege ya abiria ya C919 ya China ikionyeshwa katika Maonyesho ya Ndege ya Singapore, Februari 20, 2024. (Picha na Then Chih Wey/Xinhua) |
SINGAPORE - Ndege ya abiria ya C919 ya China imeshiriki kwa mara ya kwanza kwenye Maonyesho ya ndege ya Singapore (Singapore Airshow), ambayo yameanza Jumanne na kupangwa kuendelea hadi siku ya Jumapili wiki hii.
Ndege mbili za C919 zenye muundo mwembamba na ndege tatu za ARJ21 zilizoundwa na Shirika la Ndege ya matumizi ya kibiashara la China (COMAC) zinashiriki maonyesho hayo.
Kampuni mbili za huduma za usafiri wa anga za China, Shirika la Ndege la Tibet na Kundi la Kampuni za Maendeleo ya Usafiri na Uwekezaji wa Anga la Henan, zimetia saini oda za ndege 40 za C919 na ndege 16 za ndege za ARJ21 kwenye maonyesho hayo.
COMAC imebainisha kuwa itafanya shughuli za kutangaza ndege zake kwenye maonyesho hayo ili kuimarisha mitandao kati yake na wateja na washirika.
Timu za kufanya maonyesho ya ndege angani kutoka India, Indonesia, Australia, Jamhuri ya Korea, na ndege moja ya Airbus A350-1000 pia zinashiriki katika maonyesho hayo.
Jeshi la Anga la Singapore limetuma ndege yake ya kivita ya F-15 na helikopta ya mashambulizi ya Apache kufanya maonyesho katika maonyesho hayo.
Maonyesho hayo, yanayoshirikishwa kampuni zaidi ya 1,000, yatarajiwa kuvutia washiriki wa kibiashara 50,000 kutoka nchi na maeneo zaidi ya 50.
Pia yameweka banda kwa kampuni za vyombo vya safari za anga za China kwa mara ya kwanza, kwa mujibu wa waandaaji.
Kampuni ya Aerospace Times Feipeng kutoka Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China imeleta ndege zake za kubeba mizigo bila rubani (UAV) kwenye maonyesho hayo.
Maonyesho hayo yataendelea hadi Jumapili.
Wakulima kote China wawa na pilika nyingi za uzalishaji wa kilimo wakati Siku ya Yushui yakiwadia
Ndege C919 ya China yashiriki mazoezi ya Maonyesho ya Anga ya Singapore
Chuo Kikuu cha Kenyatta chafanya maonyesho ya dragoni wa China ili kukuza mawasiliano ya kitamaduni
Mkoa wa Xizang, China wafungua maeneo ya utalii kwa umma bila tiketi ili kuhimiza utalii
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma