Lugha Nyingine
Mapumziko ya siku nyingi zaidi ya Mwaka Mpya wa China yaleta wimbi la utalii wa Wachina (6)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 18, 2024
Tarehe 14, Februari, watalii wakitazama maporomoko ya barafu kwenye eneo la kivutio la Mlima Tianhe katika Mji wa Xingtai wa Mkoa wa Hebei, China. (Picha na Chen Lei/Xinhua) |
Kwa watu wa China, kujumuika na wanafamilia siku zote ni mambo muhimu zaidi wakati wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, lakini hivi sasa Wachina wengi zaidi wanaongeza safari za utalii kama desturi ya sikukuu hiyo.
Mwaka huu likizo ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China imedumu kwa siku nane au tisa, pamoja na siku moja ya mapumziko yanayoweza kuchaguliwa. Likizo hiyo ni ndefu zaidi kuliko likizo hiyo katika miaka iliyopita, ambayo kwa kawaida ilikuwa ya wiki moja.
Wataalamu walisema kuwa, ongezeko la matumizi ya utalii wakati wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China linaashiria mwelekeo wa kurudia kwenye hali ya juu wa shughuli za utalii nchini China mwaka 2024.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma