Lugha Nyingine
Roboti za muundo wa binadamu zaoneshwa hadharani kwa umma mjini Beijing, China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 08, 2024
Mtafiti akirekebisha roboti zenye muundo wa binadamu kwenye maabara ya teknolojia za Akili Bandia (AI), Januari 31, 2024. (Xinhua/Chen Yehua) |
Roboti zenye muundo wa binadamu za "Familia ya Q" zilizoundwa na timu ya watafiti ya Taasisi ya Otomesheni, Taasisi Kuu ya Sayansi ya China, hivi karibuni zilionyeshwa hadharani kwa umma kwa mara ya kwanza mjini Beijing.
Ikiongozwa na Qiao Hong, mwanataaluma wa Taasisi Kuu ya Sayansi ya China na mkurugenzi wa maabara muhimu ya serikali ya mifumo ya miundo mingi ya teknolojia za akili bandia, timu hiyo ya watafiti ilijenga "kiwanda kikubwa" kwa ajili ya kusanifu na kuunganisha roboti zenye muundo wa binadamu.
Mifano kadhaa za roboti hizo za "Familia ya Q" zimepata uthibitishaji wa awali wa kiufundi.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma