Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atoa salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa Wachina wote (8)
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akitembelea nyumba ya mwanakijiji na kuzungumza na familia katika kijiji cha Mji Mdogo wa Xinkou wa Tianjin, China, Feb. 1, 2024. (Xinhua/Ju Peng) |
TIANJIN - Rais wa China Xi Jinping ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) ametoa salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa watu wote wa China wakati wa ziara yake ya ukaguzi katika mji wa Tianjin, Kaskazini mwa China kuanzia siku ya Alhamisi hadi Ijumaa.
Rais Xi, amewatakia Wachina wa makabila yote, watu wa Hong Kong, Macao na Taiwan, na Wachina wanaoishi sehemu mbalimballi duniani afya njema na furaha tele katika Mwaka wa Dragoni, na ustawi wa nchi nzima ya China.
Siku ya Alhamisi asubuhi, Xi alitembelea kijiji katika Mji mdogo wa Xinkou katika Eneo la Xiqing la mji wa Tianjin.
Kuanzia mwishoni mwa Julai hadi mapema Agosti mwaka jana, mvua kubwa ilinyesha kaskazini mwa China, na kusababisha mafuriko makubwa katika Bonde la Mto Haihe, na eneo kubwa la ardhi katika hifadhi na kizuizi cha mafuriko cha bonde huko Tianjin lilifurika maji.
Akifahamishwa kuhusu athari za mafuriko hayo katika mji huo na wilaya, Xi aliingia kwenye banda la kilimo cha kisasa ili kuangalia hali ya ukuaji wa mboga za majani. Aliwauliza wakulima kwa makini juu ya urejeshaji wa mabanda hayo ya kilimo cha kisasa na upandaji upya na uuzaji wa mboga za majani.
Kisha Rais Xi alitembelea nyumba ya wanakijiji, ambapo alizungumza na watu wa vizazi vinne vya familia hiyo. Aliuliza kuhusu hasara za familia wakati wa maafa, uzalishaji na mapato yao baada ya maafa, na kufanya mahesabu kwa uangalifu wakati wa mazungumzo.
Akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha maisha ya watu, Rais Xi amesema suala hilo daima linazingatiwa na Kamati Kuu ya CPC pamoja na kamati za Chama na serikali katika ngazi zote. Pia ameelezea matumaini kuwa wanakijiji hao watafanya juhudi zao wenyewe katika kujenga upya maskani yao mazuri.
Mwaka Mpya wa Jadi wa China unapokaribia, Rais Xi, kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC, ametoa salamu zake za dhati kwa wale wote walioathiriwa na majanga na wale walioko kwenye mstari wa mbele katika ukarabati na ujenzi wa baada ya maafa.
Katika picha: Ndege yangeyange wakiwa wamepumzika kwenye Ziwa Yundang huko Xiamen China
Picha: Mandhari ya Ziwa Yundang la Xiamen, China katika ukungu
Picha:Majengo Makongwe katika Kisiwa cha Kulangsu, China ambayo yanabeba ushuhuda wa historia
Mandhari ya kushangaza ya “Barabara Kuu inayoning’inia kwenye Miteremko ya Vilima” wakati wa theluji
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma