Lugha Nyingine
Urithi wa utamaduni usioshikika unaong'aa sana: Udarizi wa Shanga za Kioo kwa mikono wa Xiamen, China (14)
Udarizi wa shanga za kioo kwa mikono Katika Mji wa Xiamen, China ni ufundi wa kazi za mikono wenye historia ya mamia ya miaka.
Katika kipindi cha mwanzo wa miaka ya 1920, Wachina walioishi ng’ambo walileta mavazi na vitu vilivyopambwa kwa shanga za kioo wakati waliporudi maskani kuwatembelea wanafamilia wao. Mafundi wa kutengeneza viatu wa Xiamen walipata ufunuo kutoka kwa vitu hivyo na kujaribu kutumia ufundi wa kudarizi shanga kwenye sehemu ya juu mbele ya viatu, ambavyo vilipendwa sana na watu. Tangu hapo udarizi wa shanga za kioo kwa mikono umeenezwa na kuendelezwa.
Hivi leo bidhaa zenye udarizi wa shanga za kioo wa Xiamen zinahusisha aina zaidi ya mia moja zikiwemo viatu, mavazi, mabegi n.k.
Tarehe 24, Mei, 2021, udarizi wa shanga za kioo kwa mikono wa Xiamen uliidhinishwa na serikali ya China kuingizwa kwenye orodha ya kundi la tano la urithi wa mali ya utamaduni usioshikika wa China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma