Lugha Nyingine
Mji wa Changzhou, China wapiga hatua katika ukuaji wa uchumi?kutokana?na sekta ya nishati mpya (8)
Picha iliyopigwa Desemba 22, 2023 ikionyesha mandhari ya usiku ya eneo la mapumziko la ziwa la chumvi la mashariki huko Changzhou, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China. (Xinhua/Ji Chunpeng) |
NANJING – Ukijulikana kama mji wa nishati mpya, Mji wa Changzhou katika Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China, umerekodi pato lake la jumla (GDP) la yuan trilioni 1.01 (dola za Kimarekani bilioni 140.8) Mwaka 2023, ikiwa ni ongezeko la asilimia 6.8 mwaka hadi mwaka, idara ya takwimu imesema Jumanne.
Ikiwa na wakazi wapatao milioni tano, Changzhou imekuwa mji wa China wenye watu wachache zaidi ukiwa na pato la jumla la Yuan zaidi ya trilioni moja, ikifuata Suzhou, Nanjing, Wuxi, na Nantong kuwa mji wa tano katika Mkoa wa Jiangsu kufikia hatua hii muhimu.
Ukiwa ni kitovu cha viwanda katika Delta ya Mto Yangtze, mji huo umevutia kampuni nyingi za kiwango cha juu za utengenezaji wa betri na magari yanayotumia nishati mapya (NEV), na kutia msukumo katika ukuaji wake wa uchumi.
Thamani ya pato la sekta ya nishati mpya katika mji huo ilifikia takriban yuan bilioni 768 mwaka jana, na mji huo unalenga kupanua thamani ya pato hadi zaidi ya yuan trilioni moja ifikapo Mwaka 2025, kwa mujibu wa Chen Jinhu, katibu wa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China ya Changzhou.
Takwimu zinaonyesha kuwa ukamilifu wa mnyororo wa viwanda wa betri huko Changzhou umefikia asilimia 97, na kushika nafasi ya kwanza nchini China, na pato lake linachukua asilimia 20 ya uwezo wa uzalishaji wa nchi hiyo.
Mji huo pia unachangia asilimia 10 ya seli na moduli za nishati ya jua zinazotengenezwa China. Mwaka 2023, ulizalisha magari yanayotumia nishati mpya zaidi ya 700,000, ikichukua asilimia 70 ya idadi ya jumla ya magari hayo yaliyozalishwa Jiangsu.
Kampuni nyingi zinazowekezwa kwa mtaji wa kigeni katika nishati mpya pia zimehamia Changzhou na kufaidika na mnyororo wa viwanda vya eneo hilo.
"Tunachagua Changzhou kwa sababu tunahitaji mahali ambapo tunaweza kupata ukuaji wa haraka sana, na Changzhou inatoa mchanganyiko wa kipekee wa miundombinu ya usambazaji," amesema Jorg Heinemann, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya EnerVenue ya Marekani, ambayo ni msambazaji wa vifaa vya kuhifadhi betri.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma