Lugha Nyingine
Kundi la Kitamaduni la China lakonga mioyo ya Waethiopia kwa maonyesho yake mazuri (3)
Wasanii na watazamaji wakifanya mazoezi ya Baduanjin, ambayo ni mchezo wa Wushu wa kujenga mwili mjini Addis Ababa, Ethiopia, Januari 23, 2024. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua) |
ADDIS ABABA – Kundi moja la utamaduni kutoka Mkoa wa Henan, katikati mwa China kimefanya maonyesho ya kuvutia katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa siku ya Jumanne ikiwa ni sehemu ya Sherehe za Mwaka Mpya wa Jadi wa China ambapo wasanii wamefanya maonesho ya michezo ya Sanaa ya sarakasi, Wushu, kubadilisha uso, ngoma za kijadi za China na Ethiopia kwa watazamaji mashabiki wengi katika Jumba la Sanaa za Maonyesho la Ethiopia.
Akiwakaribisha wageni katika maonesho hayo, Shen Qinmin, konsela katika Ubalozi wa China nchini Ethiopia, amesema Henan ni mkoa wenye utajiri wa utamaduni na historia, na kundi hilo la utamaduni litafanya "maonyesho mazuri" na kufurahisha watazamaji.
"Maonyesho ya utamaduni ni sehemu ya dhamira ya kuhimiza usawa na mawasiliano kati ya watu wa mataifa tofauti," Shen amesema.
Akizungumza katika maonesho hayo, Manyazewal Endeshaw, meneja mkuu wa Jumba la Sanaa za Maonyesho la Ethiopia, amesema Ethiopia na China zinajulikana kwa kuwa na ustaarabu wa kale wenye historia ndefu na tamaduni zenye maajabu mengi.
"Watu wa pande zote mbili wamekuwa na tamaduni na sanaa tajiri na za kupendeza, na kudhihirisha hekima na ubunifu wao," amesema Endeshaw, akisema kuwa Ethiopia itashirikiana na China na nchi nyingine katika kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja.
Kebede Kassa, mfanyakazi katika Utawala wa Jiji la Addis Ababa, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba amefurahia sana maonyesho ya kitamaduni, huku akieleza kuwa maonyesho hayo ya kitamaduni ya China amekuwa akiyapenda tangu utoto.
"Nina furaha sana kwamba kundi la utamaduni la China limekuja Ethiopia. Tukio hili limekuwa la kipekee kwa kuwa limeonyesha mchanganyiko wa tamaduni za China na Ethiopia," amesema Kassa.
Mandhari nzuri ya theluji ya Kituo cha Kuzalisha umeme kwa nishati ya Jua huko Shanxi, China
Katika Picha: Maonyesho ya taa za kijadi ya bustani ya Yuyuan mjini Shanghai, China
Watu washerehekea Sikukuu ya Timket huko Addis Ababa, Ethiopia
Sehemu ya pili ya mradi wa jengo la Kituo cha Mambo ya Fedha cha Nanjing wawekewa vifuniko
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma