Lugha Nyingine
Mavazi ya Kabila la Wahan yanayozalishwa Wilaya ya Caoxian Mkoani Shandong, China yaongoza mitindo mipya ya mavazi ya Kichina (7)
Katika miaka ya hivi karibuni, mavazi ya kijadi ya kabila la Wahan ya Hanfu yamekuwa yakipendwa sana na wateja wa China. Wakati mwaka mpya wa jadi wa China unapokaribia kuwadia, seti ya mavazi ya kuvaa kwa pamoja ya “blauzi ya salamu za mwaka mpya + sketi yenye muundo wa uso wa farasi” inayozalishwa na viwanda vya Wilaya ya Caoxian katika Mji wa Heze ulioko Mkoa wa Shandong, China inauzwa sana nchini kote, hata mahitaji yamezidi usambazaji wa bidhaa hizo sokoni.
Ikiwa ni kituo kikubwa zaidi cha ushonaji wa mavazi ya maonyesho ya jukwaani nchini China, Wilaya ya Caoxian ilianza kuzalisha mavazi hayo ya kabila la Wahan mwaka 2018, na kupata maendeleo ya kasi kupitia biashara za mtandaoni. Kwa sasa Caoxian inachukua asilimia 40 ya soko zima la mavazi ya kabila la Wahan la China. Inafahamika kuwa thamani ya mauzo ya mavazi ya Kabila la Wahan ya Wilaya ya Caoxian mwaka 2023 ilifikia Yuan bilioni 7 (sawa na Dola za Marekani milioni 978.65).
Kwa sasa kuna kampuni zinazojihusisha na biashara za mavazi ya Kabila la Wahan 2,282, maduka ya mtandaoni 13,989, na watu wanaofanya kazi husika karibia laki moja katika Wilaya hiyo. Mnyororo mzima wa viwanda hivyo unaohusisha ubunifu na ushonaji, uhifadhi wa hakimiliki ya ubunifu, na maonyesho umeshaundwa. (Picha na Zhou Linjia/People’s Daily Online)
Mandhari nzuri ya theluji ya Kituo cha Kuzalisha umeme kwa nishati ya Jua huko Shanxi, China
Katika Picha: Maonyesho ya taa za kijadi ya bustani ya Yuyuan mjini Shanghai, China
Watu washerehekea Sikukuu ya Timket huko Addis Ababa, Ethiopia
Sehemu ya pili ya mradi wa jengo la Kituo cha Mambo ya Fedha cha Nanjing wawekewa vifuniko
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma