Lugha Nyingine
Bandari kuu mbili za reli katika Mkoa wa Xinjiang zashughulikia treni za mizigo zaidi ya 70,000 za China-Ulaya
URUMQI – Lango la Alataw na Bandari ya Horgos, ambazo ni bandari kuu mbili za reli katika Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang, China, zimeshughulikia treni za mizigo zaidi ya 70,000 za China na Ulaya tangu kuanza kwao kufanya kazi. Kundi la Kampuni za Reli za China, Tawi la Urumqi limesema kwamba, hadi kufikia Januari 16 mwaka huu, Lango la Alataw lilikuwa limeshughulikia treni za mizigo 36,622 tangu Mwaka 2013, wakati Bandari kavu ya Horgos ilikuwa imeshughulikia treni 33,403 tangu Mwaka 2016.
Ili kuendeleza vyema ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, Xinjiang imeweka mkazo katika kuongeza sifa bora ya uendeshaji wa treni hizo za mizigo za China na Ulaya katika miaka ya hivi karibuni. Idadi ya treni zinazopita katika bandari kavu hizo mbili imeongezeka kwa kasi, huku wingi huo wa treni za mizigo za China na Ulaya ukichukua zaidi ya nusu ya idadi ya jumla ya China.
Hatua za kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa bandari kavu hizo mbili pia zimetekelezwa, ikiwa ni pamoja na kuboresha michakato ya uendeshaji na kupanua na kuboresha uwezo wa bandari. Kipindi cha Mwaka 2023, muda wa kusimama kwa treni za mizigo za China-Ulaya katika vituo hivi ulipunguzwa kutoka saa zaidi ya 12 hadi saa 6 hadi 8, amesema Yan Huapeng, ofisa anayefanya kazi katika Lango la Alataw.
Hivi sasa, Lango la Alataw lina njia 115 za uendeshaji wa treni za mizigo, zikitoa muunganisho wa nchi na maeneo 25. Bandari kavu ya Horgos inatoa njia 80 za uendeshaji, zinazounganisha miji na mikoa 45 katika nchi 18.
Bidhaa zinazosafirishwa kupitia bandari kavu hizi mbili zinawakilisha aina zaidi ya 200 tofauti.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma