Lugha Nyingine
Hali nzuri ya uchumi wa China inasaidia?Dunia, asema mkurugenzi mtendaji wa WEF
GENEVA - Kwa kutilia maanani mtazamo mbaya wa uchumi wa Dunia katika muda mfupi ujao, hali ya uchumi wa China inasaidia katika maeneo mengine duniani, Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Uchumi Duniani (WEF) Saadia Zahidi amesema Jumatano.
"Kama tunaangalia muda wa miaka miwili, asilimia 30 ya watu wanaona kuwa tutakabiliawa na hatari unaoweza kutokea. Linapoangalia muda wa miaka 10, karibu theluthi mbili ya watu wanaamini hivyo," Zahidi ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano yaliyofanyika kwa njia ya mtandao.
Kabla ya mkutano wake wa kila mwaka huko Davos, Uswizi, Ripoti ya Hatari ya Duniani ya WEF ya 2024 imetahadharisha kuwa habari danganyifu na habari potofu ndiyo hatari kubwa zaidi ya muda mfupi, wakati hali mbaya ya hewa na mabadiliko makubwa kwenye mifumo ya Dunia ndiyo wasiwasi kubwa kwa muda mrefu.
Ripoti hiyo pia inasema mambo maalumu katika miaka ijayo itakuwa ni kutokuwa na uhakika wa uchumi na kuongezeka kwa mgawanyiko wa uchumi na teknolojia.
Alipoulizwa kuhusu mtazamo wa uchumi wa China, Zahidi amesema: "Kutokuwa na uhakika ni hali ya jumla kwa uchumi wa nchi nyingi duniani, ikiwa ni pamoja na China. Habari njema ni kwamba China ni moja ya nchi chache zenye uchumi mkubwa duniani ambazo hazikabiliani na mfumuko wa bei, ambazo hazikabiliani na viwango vya juu vya riba kwa sasa."
"China ni moja wapo ya kundi muhimu la uchumi duniani, na kwa hivyo hali nzuri ya uchumi huo ina mwelekeo mzuri kwa Dunia nzima," ameongeza.
Kati ya tarehe 15 hadi 19 Januari, mkutano wa 54 wa kila mwaka wa WEF utafanyika Davos, Uswizi, chini ya kaulimbiu isemayo "Kujenga upya Hali ya Kuaminiana." Watu maarufu zaidi ya 300 watahudhuria mkutano wa mwaka huu, wakiwemo wakuu wa nchi na serikali zaidi ya 60, waandaaji wamesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma