Lugha Nyingine
IMF: Tanzania miongoni mwa nchi zitakazokua kwa kasi kiuchumi mwaka 2024
(CRI Online) Januari 03, 2024
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limekadiria kuwa Tanzania itakuwa na ukuaji wa kasi wa uchumi kwa mwaka 2024 likisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 12 za Afrika na 22 duniani kote katika nafasi ya juu kwa ukuaji wa uchumi kwa mwaka huu.
Ndani ya Afrika Mashariki, Tanzania inawekwa kundi moja na Ethiopia, zote mbili zinatarajiwa kuvutia uwekezaji zaidi kutoka nje.
Tanzania na Ethiopia zinabadilika kuwa nchi zenye ukuaji mzuri wa uchumi katika eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Uzalishaji wa ndani na maendeleo ya viwanda vimetajwa kuwa vichocheo muhimu vya ukuaji chanya katika nchi hizo mbili.
Kwa mujibu wa shirika hilo, makadirio ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania na Ethiopia mwaka 2024 ni asilimia 6.1 na 6.2 mtawalia.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma