Lugha Nyingine
Bandari ya Manzhouli ya China yaweka Rekodi Mpya ya Kihistoria ya Safari za Treni za Mizigo za China-Ulaya Mwaka 2023
Kreni ikipakia makontena kwenye Stesheni ya Reli ya Manzhouli mjini Manzhouli, Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China, Machi 15, 2023. (Xinhua/Bei He)
HARBIN - Manzhouli, bandari kubwa zaidi ya nchi kavu ya China, imeshughulikia safari 5,001 za treni za mizigo zinazotoa huduma kati ya China na Ulaya Mwaka 2023, ikiwa ni ongezeko la asilimia 3 ikilinganishwa na Mwaka 2022, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Kundi la Kampuni za Reli za China, Tawi la Harbin.
Hii ni mara ya kwanza kwa idadi hiyo kuzidi 5,000 ndani ya mwaka mmoja. Idadi ya safari za treni za mizigo za China na Ulaya na bidhaa zinazosafirishwa kupitia Manzhouli zimepata ukuaji endelevu kwa miaka 10 mfululizo.
Mwaka jana, treni za mizigo za China-Ulaya zilisafirisha makontena 540,000 za shehena za mizigo zenye urefu wa futi ishirini (TEUs) kupitia bandari hiyo, ikiwa ni ongezeko la asilimia 16 mwaka hadi mwaka.
Hadi sasa, njia 21 za treni za mizigo za China-Ulaya zimepita bandari hiyo iliyoko Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China, na kuunganisha nchi 13 zikiwemo Poland, Ujerumani na Ubelgiji na miji 60 ya China. Mizigo inayosafirishwa inajumuisha aina 12 kuu, kama vile mahitaji ya kila siku, mashine za viwandani na bidhaa za kilimo.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma