Lugha Nyingine
China yasema ina uhakika wa kudumisha kithabiti biashara ya nje na sehemu ya soko la kimataifa Mwaka 2023
Picha hii iliyopigwa Januari 10, 2023 ikionyesha mandhari ya eneo la Lujiazui la Majaribio ya Biashara Huria la China mjini Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Fang Zhe)
BEIJING - China ina uhakika wa kudumisha kiwango chake cha biashara ya nje na utulivu wa jumla wa mgao wake kwenye soko la kimataifa kwa mwaka huu wa 2023, He Yadong, msemaji wa Wizara ya Biashara ya China ameuambia mkutano na waandishi wa habari mjini Beijing siku ya Alhamisi.
Amesema biashara ya nje ya China imeonyesha uhimilivu mkubwa kiasi mwaka huu, ikishinda athari za kupungua kwa mahitaji ya nje, hali ya kushuka kwa bei, na msingi wa juu wa mwaka jana.
Akitazamia mbeleni Mwaka 2024, He amesema kuwa China inakabiliwa na hali ya kutokuwa na uhakika katika mazingira ya nje, lakini pia kushuhudia kuongezeka kwa sababu nzuri kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi.
Msemaji huyo amesema, gawio la ufunguaji mlango wa China litaendelea, na bidhaa mpya pamoja na hali mpya ya biashara zitaonesha uwezo zaidi wa kifursa katika biashara ya nje ya China. "Kwa kuungwa mkono na sera mbalimbali za kuleta utulivu wa uchumi na biashara ya nje pamoja na juhudi za pamoja za kampuni za biashara, China ina uhakika wa kudumisha mwelekeo wa kurudisha hali nzuri siku hadi siku katika biashara yake ya nje," amesema He.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma