Lugha Nyingine
Kamati Kuu ya Kijeshi ya Chama cha Kikomunisti cha China yafanya hafla ya kuwapandisha vyeo kuwa vya ujenerali
Xi Jinping na viongozi wengine wa jeshi wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa viongozi wa jeshi waliopandishwa vyeo kuwa vya ujenerali. (Picha na Li Gang/Xinhua)
Tarehe 25, hafla ya Kamati Kuu ya Kijeshi ya Chama cha Kikomunisti cha China (CMC) ya kuwapandisha vyeo kuwa vya ujenerali maofisa viongozi wa jeshi ilifanyika kwenye Jengo la Agosti Mosi hapa Beijing, China. Xi Jinping, ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo alishiriki kwenye hafla hiyo.
Hafla ya kupandishwa vyeo ilianza saa 5 asubuhi. Naibu mwenyekiti wa CMC Bw. Zhang Youxia alitangaza amri iliyotiwa saini na mwenyekiti wa kamati kuu ya kijeshi Xi Jinping ya kuwapandisha vyeo maofisa viongozi hao wa jeshi. Naibu mwenyekiti mwingine wa CMC Bw. He Weidong aliongoza hafla ya kupandishwa cheo kwa maofisa hao viongozi.
Maofisa viongozi wa jeshi waliopandishwa vyeo ni Wang Wenquan, kamisaa wa siasa wa Eneo la Kivita la Kusini la China, pamoja na Hu Zhongming, amri jeshi mkuu wa Jeshi la Majini la China.
Xi na viongozi wengine walipiga picha pamoja na maofisa viongozi hao baada ya hafla kumalizika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma