Lugha Nyingine
Meli kubwa zaidi duniani ya kifahari ya abiria ya "ro-ro" No. 2 yapewa jina na kuanza safari rasmi kutoka Guangzhou, China (4)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 20, 2023
Meli kubwa zaidi duniani ya kifahari ya abiria ya “ro-ro” No. 2 (“roll-on/roll-off”) yenye njia za magari za mita 3800, na yenye uwezo wa kubeba abiria 2500 iliyoundwa na Shirika la Uundaji wa Meli la China (CSSC) kwa ajili ya Kampuni ya Usafiri wa Majini ya Italia, MOBY Line, “MOBY LEGACY” imeanza rasmi safari yake kutoka Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China siku ya Jumanne, Tarehe 19, Desemba. Meli hiyo ni moja kati ya meli kubwa zaidi duniani za kifahari za abiria aina ya “ro-ro”. Baada ya kukabidhiwa kwa kampuni husika ya Italia, meli hiyo itatoa huduma za usafiri kati ya miji ya Genoa, Olbia na Livorno nchini Italia.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma