Lugha Nyingine
Kenya yazindua mkakati wa kuimarisha biashara ya mtandaoni
(CRI Online) Desemba 14, 2023
Kenya imezindua mkakati wa taifa wa biashara ya mtandaoni, katika jitihada za kurahisisha sekta hiyo inayokua kwa kasi kufuatia ustawi wa uchumi wa kidijitali.
Katika uzinduzi huo, Waziri wa habari, mawasiliano na uchumi wa kidijitali wa Kenya Eliud Owalo, amesema mkakati huo unalenga kuifanya Kenya kuwa kitovu cha kikanda cha biashara ya mtandaoni, kuongeza biashara ya ndani na nje ya nchi na kuongeza mapato na ajira.
Amesema mkakati huo utaimarisha upatikanaji wa masoko ya kimataifa kwa bidhaa na huduma za Kenya, hasa kwa kampuni ndogo na za kati kupitia biashara ya mtandaoni.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma