Lugha Nyingine
Ukuaji wa uchumi wa nchi za Afrika Mashariki huenda ukapungua mwaka 2024
Kampuni ya kimataifa ya ukaguzi wa mahesabu Deloitte imesema, nchi za kanda ya Afrika Mashariki zinaweza kukabiliwa na ukuaji mdogo wa uchumi mwaka 2024 baada ya kukabiliana na changamoto zilizojitokeza mwaka huu.
Katika ripoti yake iliyotolewa Jumanne jijini Nairobi, Kenya, kampuni hiyo imetoa makadirio ya kina ya mtazamo wa uchumi kwa hivi sasa katika kanda hiyo, uliokabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kushuka kwa thamani ya sarafu za nchi hizo, kuongezeka kwa gharama za maisha, ukame, ongezeko la deni la umma na mvutano wa siasa za kijiografia.
Mshauri wa masuala ya uchumi wa Afrika katika kampuni hiyo, Tewodros Sisay amesema, ukuaji wa uchumi wa Afrika Mashariki unatarajia kurejea tena mwaka 2024, ukiwa na kuongezeka kwa kiwango cha asilimia 6.5.
Amesema ongezeko hilo litatokana na kuimarika kikamilifu kwa sekta ya huduma, kuboreshwa kwa biashara ya nje na kuongezeka kwa matumizi binafsi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma