Lugha Nyingine
Habari Picha: Banda la China kwenye Mkutano wa Tabianchi wa COP28 Dubai, UAE (3)
Banda la China kwenye Mkutano wa 28 wa Nchi Watia saini wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) lilifunguliwa rasmi Novemba 30 katika Mji wa Maonyesho wa Dubai, Falme za Kiarabu. Banda hilo limekuwa likiandaa mfululizo wa shughuli za pembezoni mwa mkutano huo katika siku tisa zenye mada mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mikutano miwili maalum, wakati wa wiki mbili za Mkutano huo.
Idara husika za serikali, taasisi za utafiti, mashirikisho ya viwanda, kampuni na mashirika yasiyo ya kiserikali yatashiriki kwenye shughuli hizo, mada za shughuli hizo zinahusu sera na hatua za mwitikio wa China juu ya mabadiliko ya tabianchi, ushirikiano wa kimataifa wa tabianchi, maendeleo ya kijani ya kutoa kaboni chache, kubadilisha muundo wa nishati, maendeleo ya kidijitali, na mambo ya fedha yanayosaidia miradi isiyotoa uchafuzi kwa mazingira.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma