Lugha Nyingine
Misri yahitimisha maonyesho ya dhahabu huku kukiwa na ongezeko la mahitaji ya dhahabu (2)
Muonyeshaji bidhaa akionyesha mapambo ya dhahabu kwenye Maonyesho ya Nebu ya Dhahabu na Vito mjini Cairo, Misri, Novemba 28, 2023. (Xinhua/Ahmed Gomaa) |
CAIRO - Misri imehitimisha Maonyesho ya tatu ya Nebu ya Dhabu na Vito siku ya Jumanne huku kukiwa na kupanda kwa bei ya dhahabu na mahitaji yanayoongezeka, wakati nchi hiyo ikikabiliwa na uhaba wa dola ya Marekani, kushuka kwa thamani ya fedha yake na mfumuko mkubwa wa bei.
Ehab Wassef, mkuu wa kitengo cha sekta ya dhahabu katika Shirikisho la Viwanda vya Misri, amesema bei ya dhahabu imepanda kimataifa hadi kuzidi dola 2,000 za Marekani kwa wakia, hali ambayo imejidhihirisha katika bei zake nchini Misri.
"Hivi karibuni tumekuwa na mahitaji makubwa ya dhahabu miongoni mwa raia na kampuni za Misri kwa ajili ya kuweka akiba na uwekezaji," Wassef ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua, akinukuu ripoti ya hivi karibuni ya Baraza la Dhahabu la Dunia kwamba "Wamisri walinunua karibu tani 46.3 za dhahabu katika miezi tisa ya kwanza ya Mwaka 2023 ".
Wakati wa maonyesho hayo, kampuni zaidi ya 150 zilionyesha bidhaa za dhahabu, sarafu na dhahabu bapa, bidhaa mbalimbali za vito, na mashine na zana husika.
Tarek Al-Taroty, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Dhahabu ya New Egypt, moja ya kampuni kubwa zaidi zilizoshiriki maonyesho hayo, amesema kuwa dhahabu imethibitika kuwa "mahali salama" na "fedha inayotambulika kimataifa" huku kukiwa na changamoto na misukosuko ya kiuchumi.
Amesema kuwa shauku kubwa ya kupita kiasi ya kununua dhahabu nchini Misri, hasa sarafu za dhahabu na dhahabu bapa, inatokana zaidi na kupanda kwa kiwango cha ubadilishaji wa dola ya Marekani dhidi ya pauni ya Misri.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma