Lugha Nyingine
Tembelea ndani ya jumba la Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya Mnyororo wa Ugavi ya China (7)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 27, 2023
Picha iliyopigwa tarehe 26, Novemba ikionesha banda la kampuni ya Bloomega Biotech kwenye eneo la mnyororo wa ugavi wa maisha yenye afya la Maonesho ya Kimataifa ya Mnyororo wa Ugavi ya China. |
Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya Mnyororo wa Ugavi ya China yenye kaulimbiu ya “Kuunganisha dunia na kujenga mustakabali wa pamoja” yatafanyika kuanzia Novemba 28 hadi Desemba 2 mjini Beijing, China. Haya ni maonesho ya kwanza ya ngazi ya taifa duniani yanayohusu mnyororo wa ugavi. Maonesho hayo yanachukua eneo la maonesho la ukubwa wa mita za mraba laki moja, na yataweka maeneo ya mnyororo wa ugavi wa magari, kilimo cha kijani, nishati mbadala, teknolojia ya kidijitali, maisha yenye afya na huduma za mnyororo wa ugavi. Hadi hivi sasa, kazi ya maandalizi ya maonesho hayo inaendelea kwa utaratibu kwenye Jumba la Shunyi la Kituo cha Kimataifa cha Maonyesho cha China.
(Picha na Ren Chao/Xinhua)
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma