Lugha Nyingine
Reli mpya inayounganisha miji maarufu ya kitalii ya Lijiang na Shangri-la Kusini Magharibi mwa China yafunguliwa (5)
Picha hii ikionesha eneo la mbele ya Stesheni ya reli ya Shangri-la katika Mkoa wa Yunnan, Kusini-Magharibi mwa China. (Xinhua/Hu Chao) |
KUNMING - Reli ya Lijiang-Shangri-la inayounganisha miji ya Lijiang na Shangri-la, ambayo ni miji yenye vivutio maarufu kwa watalii katika Mkoa wa Yunnan, Kusini-Magharibi mwa China, imefunguliwa kwa matumizi ya umma siku ya Jumapili, kwa mujibu wa serikali ya mtaa wa eneo husika ambapo inatarajiwa kushuhudia muda wa kusafiri kwa kasi zaidi kati ya miji hiyo miwili ukiwa saa 1 na dakika 18.
Reli hiyo yenye urefu wa kilomita 139 pia inaunganisha Mji wa Shangri-la wa Eneo linalojiendesha la Kabila la Watibet la Diqing, na mji wa Kunming wa mkoa wa Yunnan.
Kampuni ya Kundi la Reli la Kitaifa la China imeeleza kuwa, Njia hiyo mpya ya reli itasaidia kuboresha usafiri katika maeneo ya makabila madogo, hali ambayo inahimiza mshikamano ya makabila, kuimarisha hali ya utulivu wa mipaka, na kuendeleza maendeleo yenye ubora wa juu ya Yunnan.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma