Lugha Nyingine
Mradi wa “Sinema ya Nuru” wa Chuo Kikuu cha Mawasiliano ya Habari cha China wasifiwa kuwa mradi bora zaidi wa kuondoa umaskini (4)
Mradi wa “Sinema ya Nuru” unawazawaidia wanafunzi wenye ulemavu wa macho filamu ya hali isiyo na vizuizi kwao katika Wilaya ya Zhongyang ya Mji wa Lvliang ya Mkoa wa Shanxi wa China. |
Tarehe 1, Novemba 2023, “ Kongamano la Wenzi wa Kuondoa Umaskini Duniani 2023” lilifanyika hapa Beijing, ambapo ilitolewa orodha ya miradi 104 iliyopata tuzo ya “Shughuli ya Nne ya Kimataifa ya Kukusanya Miradi ya Kuondoa Umaskini” lililoandaliwa pamoja na Kituo cha kimataifa cha Kusaidia Kuondoa Umaskini cha China, Benki ya Dunia (WB), Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo ya Kimataifa, Shirika la Mpango wa Chakula wa Dunia la Umoja wa Mataifa (WFP), Benki ya Maendeleo ya Asia (ADB) na Kituo cha Habari cha Mtandao wa Intaneti cha China.
Katika miradi 898 iliyokusanywa kwenye shughuli hiyo, mradi wa Chuo Kikuu cha Mawasiliano ya Habari cha China wa “Kuhimiza Ustawishaji wa Vijiji kwa Msaada wa Utamaduni: Sinema ya Nuru, mradi wa utengenezaji filamu ya hali isiyo na vizuizi kwa watu wenye ulemavu na uenezi bila ya kutafuta faida chini ya ushirikiano wa chuo kikuu na kampuni” ulipata tuzo ya “mradi bora zaidi wa kuondoa umaskini” wa shughuli hiyo.
Mradi wa “Sinema ya Nuru” ya utengenezaji filamu ya hali isiyo na vizuizi na uenezi bila ya kutafuta faida ulianzishwa mwaka 2017 na Chuo Kikuu cha Mawasiliano ya Habari cha China, Kampuni ya Televisheni ya Gehuayouxian ya Beijing na Kampuni ya Filamu kwenye Televisheni ya Dongfangjiaying. Hadi hivi sasa mradi huo umemaliza kutengeneza filamu ya hali isiyo na vizuizi zaidi ya 500.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma