Lugha Nyingine
Tamasha la Mwaka la Utamaduni laongeza maafikiano ya tamaduni za Wachina na Wanigeria (3)
ABUJA - Mdundo wa ngoma za Nigeria ukiambatana na sauti maridadi za ala za muziki wa Kichina, umeundwa kama muziki wa Symphony ambao uliambatana na moyo wa mshikamano wa China na Nigeria za kupongeza tamaduni za nchi hizi mbili kwenye Tamasha la Mwaka wa Utamaduni wa China na Nigeria lilipofanyika Jumanne iliyopita.
Wanafunzi kutoka shule 12 za umma katika mji mkuu Abuja wa Nigeria wakiwa wamevalia mavazi ya kuvutia ya kitamaduni ya China na Nigeria, wakiwa na ala maarufu, walikusanyika kwenye Kituo cha Utamaduni cha China, mahali tamasha hilo la mwaka wa utamaduni lilipofanyika, ili kushindana kati yao katika kucheza ngoma za China na ngoma za Nigeria.
Tamasha hilo lililoandaliwa na Ubalozi wa China nchini Nigeria na Bodi ya Elimu ya Sekondari ya Mji Mkuu la Nigeria (FCT), ni matokeo ya juhudi za Klabu ya Kona ya Lugha ya Kichina, klabu iliyoundwa kwa madhumuni ya masomo ya ziada na shule za sekondari zinazomilikiwa na serikali huko Abuja, ili kujifunza na kubadilishana mawazo kuhusu utamaduni wa China.
"Hili ni tukio la kusisimua sana kwangu. Nina furaha siyo tu kuwa nimeshuhudia hili lakini pia nimeshindana na kushinda," amesema Gift Paul, mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Siku ya Serikali huko Dutse, kitongoji cha Abuja. Huyu ni sehemu kikundi kilichoshinda tuzo ya kwanza kwa shule yake katika mashindano yaliyofanyika mwaka jana.
Wakiwasilisha tamasha kubwa kwa watazamaji walioshuhudia kuongezeka kwa mawasiliano kati ya watu wa China na Nigeria, wachezaji ngoma wadogo walikuwa wepesi kati ya miondoko ya ngoma za China na miondoko ya kusisimua na yenye nguvu ya ngoma za Nigeria. Makofi ya shangwe yaliyofuata kila tendo siyo tu kwa ajili ya maonyesho hayo ya kuvutia bali pia kwa ajili ya daraja lililojengwa kati ya nchi hizo mbili kupitia lugha ya ulimwengu ya sanaa na utamaduni.
Konseli wa utamaduni katika Ubalozi wa China nchini Nigeria Bw.Li Xuda amesema, mawasiliano ya kitamaduni kati ya nchi hizo mbili yamekuzwa sana, na Tamasha la Mwaka wa Utamaduni wa China na Nigeria hadi sasa limekuwa "chapa maarufu ya kitamaduni."
Habari ya picha ya wanandoa wapanda msitu katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
Mandhari ya majira ya Mpukutiko katika Kaunti ya Gongbo'Gyamda mjini Nyingchi, Mkoa wa Tibet, China
Tamasha la 15 la Mitindo ya Mavazi na Uanamitindo la Afrika lafanyika nchini Benin
Mandhari ya Hifadhi ya Taifa ya Mazingira Asilia ya Milima ya Altun katika Mkoa wa Xinjiang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma