Lugha Nyingine
Chai nyeupe katika Mkoa wa Guizhou, China yasifiwa na waandishi wa habari wa nchi za Eurasia (2)
Waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya nchi za Eurasia wakijadiliana na Gong kuhusu utamaduni wa chai. (Picha na Yang Qian/People’s Daily Online) |
Hivi karibuni shughuli ya "kupika chai kwa stovu" ilifanyika kando ya Ziwa Baihua katika mji mdogo wa Zhuchang ulioko Mji wa Guiyang katika Mkoa wa Guizhou nchini China, ambapo waandishi wa habari kutoka Kazakhstan, Uzbekistan, Kyrgyzstan, Georgia na Armenia walikunywa chai huku wakizungumzana. “Shamba la Chai la Shenque siyo tu lina mazingira mazuri ya bustani, bali pia chai inayozalishwa ina ladha ya kipekee,” amesifu mwandishi wa habari kutoka Kazakhstan Arsen Nurtazin.
“Kuzalisha chai salama, nzuri kwa afya na safi ni lengo letu,” amesema Gong Rui, mwenyekiti wa bodi ya Shamba la Chai la Shenque. Chai nyeupe kutoka shamba hilo siyo tu imeingia kwenye masoko ya Beijing, Shanghai, Guangzhou na miji mingine nchini China, lakini pia imeuzwa nchini Argentina, Laos na nchi mbalimbali duniani, na hata imekuwa chai ya heshima inayotumiwa na familia ya kifalme ya Nchi ya Falme za Kiarabu (UAE). “Kuna nyumba nyingi za kunywea chai katika nchi yetu, na sehemu kubwa ya majani ya chai huagizwa kutoka China. Labda siku moja nitaweza kunywa chai kutoka Shamba la Chai la Shenque nchini Armenia,” amesema Paruir Siniavskii, mwandishi wa habari wa shirika la habari la Armenia.
Kama bidhaa muhimu iliyokuwa ikitembezwa katika njia ya kale ya hariri, Chai imeanza safari ya kisasa ya “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Licha ya hayo, chai imekuwa “injini ya kijani” ya kuhimiza ustawishaji wa vijiji mkoani Guizhou. Mkoa huo una bustani za chai zenye eneo lenye ukubwa wa mu zaidi ya milioni 700 (sawa na hekta 466,667). Katika miaka ya hivi karibuni, ubora, ufanisi na uwezo wa ushindani wa sekta ya chai ya Guizhou umeendelea kuongezeka, na sekta ya chai ya mkoa huo hatua kwa hatua imeanza safari ya “kutengeneza faida kwa kampuni huku ikinufaisha wakazi”.
Habari ya picha ya wanandoa wapanda msitu katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
Mandhari ya majira ya Mpukutiko katika Kaunti ya Gongbo'Gyamda mjini Nyingchi, Mkoa wa Tibet, China
Tamasha la 15 la Mitindo ya Mavazi na Uanamitindo la Afrika lafanyika nchini Benin
Mandhari ya Hifadhi ya Taifa ya Mazingira Asilia ya Milima ya Altun katika Mkoa wa Xinjiang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma