Lugha Nyingine
Msumbiji yatafuta?ushirikiano wa karibu wa kibiashara na uwekezaji na China
Waziri Mkuu wa Msumbiji Adriano Maleiane akizungumza kwenye hafla ya utangazaji wa fursa za uwekezaji mjini Wuhan, China, Oktoba 20, 2023. (Xinhua/Cheng Min) |
Waziri Mkuu wa Msumbiji Adriano Maleiane ameeleza matumaini ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na China katika sekta mbalimbali kwenye hafla ya kutangaza fursa za uwekezaji iliyofanyika Ijumaa mkoani Hubei, China.
Katika hotuba aliyotoa kwenye hafla hiyo, Waziri Mkuu Maleiane amesisitiza nguvu ya fursa za kiuchumi ya Msumbiji na matumaini yake kwa nchi zote mbili kuimarisha ushirikiano katika sekta za kilimo, utalii, nishati na maendeleo ya miundombinu ili kuhimiza uchumi wa nchi hiyo kuwa vyanzo mbalimbali. Maofisa wa Serikali ya Msumbiji na wawakilishi wa makampuni zaidi ya 50 walihudhuria hafla hiyo.
Takwimu zilizotolewa kwenye hafla hiyo na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Msumbiji Bw Silvino Moreno, China ni miongoni mwa wawekezaji 10 wakubwa wa Msumbiji, ikiwa na miradi 166 iliyoidhinishwa kati ya Mwaka 2017 na 2022, na kuleta fursa za ajira zaidi ya 19,000. Thamani ya jumla ya uwekezaji imezidi dola bilioni 1 za Kimarekani, ambapo zaidi ya dola milioni 700 ni uwekezaji wa moja kwa moja.
“Sehemu kubwa ya uwekezaji huu uko katika sekta ya viwanda, ikifuatiwa na ujenzi na huduma”, Amesema Bwana Moreno, huku akiongeza kuwa Msumbiji inatarajia uwekezaji zaidi kutoka China katika sekta za kilimo, viwanda, miundombinu, na uchukuzi.
Habari Picha: Watu wakitembelea Mlima Huashan katika Mkoa Shaanxi, Kaskazini Magharibi mwa China
Mandhari ya Ziwa Kanas katika Eneo la Altay, Mkoa wa Xinjiang, China wakati wa majira ya mpukutiko
Katika Picha: Mandhari ya magenge kwenye Mto Manjano huko Henan, China
Bahari ya Maua ya Mlima Jing katika Mji wa Hangzhou wa Zhejiang, China yakaribisha watalii
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma