Lugha Nyingine
Mkutano wa Kilele wa Ukanda Mmoja, Njia Moja wafunguliwa
(CRI Online) Oktoba 18, 2023
Mkutano wa Kilele wa Tatu wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja umefunguliwa leo tarehe 18 Oktoba mjini Beijing, ambapo rais Xi Jinping wa China amehudhuria na kutoa hotuba.
Mkutano huo wa kilele ni shughuli muhimu zaidi ya kidiplomasia inayofanyika nchini China mwaka huu. Kauli mbiu ya Mkutano huo ni “Kujenga pamoja ‘Ukanda Mmoja, Njia Moja’ kwa sifa ya juu, kushirikiana ili kutimiza maendeleo na ustawi wa pamoja”. Wawakilishi kutoka zaidi ya nchi 140 na zaidi ya mashirika 30 ya kimataifa wanashiriki kwenye mkutano huo, ikiwa ni pamoja na viongozi wa nchi husika, wakurugenzi wa mashirika ya kimataifa, mawaziri, na wadau kutoka sekta ya viwanda na biashara, taasisi za akademia na asasi za kijamii.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma