Lugha Nyingine
IMF yakadiria "kuyumba" kwa uchumi wa Dunia Mwaka 2023 (2)
Picha iliyopigwa Oktoba 10, 2023 ikionyesha mkutano na waandishi wa habari kuhusu ripoti ya Mtazamo wa Uchumi wa Dunia ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) huko Marrakesh, Morocco, Oktoba 10, 2023. (Xinhua/Huo Jing) |
MARRAKECH - Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limekadiria ukuaji wa uchumi duniani kupungua kutoka asilimia 3.5 Mwaka 2022 hadi asilimia 3 mwaka huu katika ripoti yake ya Mtazamo wa Uchumi wa Dunia iliyotolewa Jumanne kwenye Mikutano ya kila Mwaka ya Mwaka 2023 ya Benki ya Dunia na IMF inayoendelea katika Jiji la Marrakesh, Morocco.
"Uchumi wa Dunia unasuasua, si kukimbia," inasomeka ripoti hiyo mpya ya IMF yenye kichwa kisomekacho "Kuzipita Tofauti za Dunia"
Katika ripoti hiyo, IMF imekadiria ukuaji wa uchumi wa asilimia 2.9 kwa Mwaka 2024, ikishusha makadirio yake ya awali ya ukuaji wa asilimia 3 iliyoyatoa Mwezi Julai kutokana na kuimarika polepole kwa uchumi kuliko ilivyotarajiwa kutoka kwenye athari za janga la UVIKO-19 na vita nchini Ukraine.
“Kwa kurejea nyuma, uchumi wa Dunia umekuwa ukihimili usumbufu wa soko la nishati na chakula unaosababishwa na vita, pamoja na kukazwa kwa hali ya mambo ya fedha ya kimataifa isiyotokea awali ili kukabiliana na mfumuko wa bei wa miongo kadhaa,” inasema ripoti hiyo.
Hata hivyo, ripoti hiyo ina mashaka kwamba ukuaji wa uchumi unaendelea kuwa wa polepole na usio sawa kwa pande zote, huku kukiwa na tofauti zinazoongezeka za kimataifa.
Kushuka kwa uchumi kunaonekana zaidi katika nchi zilizoendelea kuliko katika nchi za masoko yanayoibukia na zile zinazoendelea. Kwa nchi zilizoendelea, kushuka kwa uchumi kunakotarajiwa ni kutoka asilimia 2.6 Mwaka 2022 hadi asilimia 1.5 Mwaka 2023 na asilimia 1.4 Mwaka 2024, huku uchumi wa Marekani unaimarika zaidi kuliko ulivyotarajiwa, lakini ukuaji wa uchumi ni dhaifu kuliko ulivyotarajiwa katika eneo linalotumia sarafu ya Euro barani Ulaya.
Nchi na maeneo yenye masoko yanayoibukia na zile zinazoendelea zinakadiriwa kushuhudia kupungua kwa kiwango cha ukuaji wa uchumi kutoka asilimia 4.1 Mwaka 2022 hadi asilimia 4 Mwaka 2023 na 2024, pamoja na marekebisho ya kupungua kwa asilimia 0.1 Mwaka 2024.
Wakati huo huo, IMF imeonya kwamba kuongezeka kwa mgawanyiko wa siasa za kijiografia haitamaanisha tu kusababisha gharama kubwa kwa ustawi wa dunia lakini pia kutazuia ushirikiano wa kimataifa katika kutoa bidhaa muhimu za umma, kama vile kupambana na mabadiliko ya tabianchi na majanga ya baadaye ya magonjwa ya maambukizi na kuhakikisha nishati na usalama wa chakula.
Kuhusu mgogoro unaoendelea kati ya Palestina na Israel, mwanauchumi mkuu wa IMF Pierre-Olivier Gourinchas amesema ni "mapema sana" kutathmini athari zake katika ukuaji wa uchumi wa Dunia, na IMF "inafuatilia hali hiyo kwa karibu."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma