Lugha Nyingine
Mzigo wa bidhaa zinazochukuliwa kupita mlango wa meli wa Magenge Matatu waweka rekodi mpya
Picha hii iliyopigwa angani Tarehe 8, Oktoba, 2023 ikionesha meli zikipita mlango wa meli wa Bwawa la Magenge Matatu huko Yichang, Mkoa wa Hubei katikati ya China. (Picha na Wang Gang/Xinhua) |
Mzigo wa bidhaa zinazochukuliwa kupita mlango wa meli wa Bwawa la Magenge Matatu, ambalo ni sehemu ya mradi mkubwa zaidi wa kuzalisha umeme kwa nishati ya maji duniani, umefikia uzito wa jumla wa tani milioni 127 katika robo tatu za kwanza za mwaka huu, ikiongezeka kwa asilimia 10.02 kutoka kwenye kiwango cha wakati kama huo mwaka jana, takwimu zimeonesha siku ya Jumapili.
Takwimu hizo kutoka Mamlaka ya Uchukuzi wa Maji ya Magenge Matatu zinaonesha kuwa, hii ni mara ya kwanza kwa mlango huo wa meli kuzidi kiwango cha tani milioni 120 katika robo tatu za kwanza za mwaka katika uendeshaji wake wa miongo miwili.
Mlango huo wa meli umeshughulikia meli 32,000 za mizigo katika kipindi cha mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu, kwa mujibu wa mamlaka hiyo.
Mlango huo wa meli ni sehemu ya mradi wa Magenge Matatu, ambao ni mfumo wa udhibiti maji unaofanya kazi mbalimbali kwenye Mto Yangtze, mto mrefu zaidi wa China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma