Lugha Nyingine
Mafanikio ya China yahamasisha Afrika kutafuta njia ya kujitegemea ya maendeleo (2)
JOHANNESBURG - Kwa kuhamasishwa na maendeleo ya China kwa miongo kadhaa, nchi nyingi zaidi za Afrika zinatafuta kufuata njia za maendeleo zinazoendana na hali ya nchi husika.
Kwenye Mazungumzo ya Viongozi wa China na Afrika yaliyofanyika mjini Johannesburg, Afrika Kusini mwishoni mwa Agosti, Rais Xi Jinping wa China kwa mara nyingine tena alihimiza nchi za Afrika kutafuta njia ya maendeleo inayofaa zaidi kwa Afrika.
"Watu wa Afrika ndiyo wana sauti zaidi juu ya njia ipi inayofaa zaidi Afrika. Kuendeleza maendeleo ya kisasa kupitia ushirikiano ni chaguo la kujitegemea linalofanywa na nchi na watu wa Afrika," Rais Xi alisema.
Tichaona Zindoga, mwanzilishi na mkurugenzi wa taasisi ya Wanafikra Bingwa ya Kituo cha Habari na Rasilimali cha Ruzivo nchini Zimbabwe, amesema kuwa mbinu zenye mwelekeo wa Nchi za Magharibi hazijaisaidia vyema Afrika baada ya uhuru.
"Usanifu na muundo wa uchumi wa kikoloni ulifaa kuendana na mtindo wa Nchi za Magharibi na kuwafaa watu wachache tu waliokuwa wa tabaka la ubepari wa wakati huo," amesema.
Melaku Mulualem, mtafiti mwandamizi wa uhusiano wa kimataifa na diplomasia katika Taasisi ya Masuala ya Kimkakati ya Ethiopia, amesema nchi za Afrika zimeanza kuchunguza ujanibishaji wa njia za maendeleo zinazofaa kwa hali zao wenyewe.
Paul Frimpong, mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Af?ika na China cha Sera na Ushauri, ambayo ni taasisi wanafikra mabingwa yenye makao yake makuu nchini Ghana amesema njia ya China ya maendeleo ya amani inafaa kwa Bara la Afrika kujifunza, ambalo lina historia sawa na China, lakini bado linakabiliwa na machafuko na misukosuko katika baadhi ya maeneo.
"Hii ni aina ya ufahamu ambao ninapata kutoka kwenye maendeleo ya kisasa ya China," amesema.
Naye Benjamin Akuffo, kaimu mhariri wa The Insight, gazeti la Ghana amesema nchi za Afrika zinahitaji kupanua ukuaji wa viwanda, kuongeza maendeleo ya miundombinu na mitandao ya biashara na kuwekeza katika rasilimali watu kama ilivyofanya China.
Kwenye mazungumzo hayo mjini Johannesburg, Rais Xi alitangaza kuwa China itazindua Mpango wa Kusaidia Maendeleo ya Viwanda barani Afrika, Mpango wa China Kusaidia Kilimo cha Kisasa cha Afrika na Mpango wa Ushirikiano kati ya China na Afrika kuhusu Maendeleo ya Vipaji, ambao ulikaribishwa kwa furaha na viongozi wa Afrika.
Akuffo anataja mipango hiyo pamoja na ule wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) kuwa imekuwa na mchango muhimu katika kusaidia Afrika kufikia Ajenda ya 2063 ambayo inahimiza kufikia maendeleo endelevu na jumuishi ya kijamii na kiuchumi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma