Lugha Nyingine
Mkoa wa Liaoning nchini China watia saini uwekezaji wa dola za Kimarekani zaidi ya bilioni 80 kwenye maonyesho ya kimataifa
SHENYANG – Miradi ya uwekezaji wenye thamani ya yuan zaidi ya bilioni 586 (kama dola bilioni 81.7 za Kimarekani) imetiwa saini kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Uwekezaji na Biashara ya Liaoning Mwaka 2023, yaliyoanza Jumatatu katika Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China.
Maonyesho hayo yamesaidia mkoa huo kutia saini miradi jumla ya 271 na wawekezaji baada ya hafla ya ufunguzi huko Shenyang, mji mkuu wa mkoa huo, amesema mratibu wa maonyesho hayo.
Takriban wahudhuriaji 3,000 kutoka ujumbe wa kiuchumi na kibiashara wa ndani na nje ya China, pamoja na kampuni zilizo kwenye orodha ya Kampuni Bora 500 duniani na mashirikisho ya wafanyabiashara watashiriki katika maonyesho hayo ya siku tatu.
Yakiwa yanajikita katika mada ya kukuza mafanikio mapya katika ustawi wa kiuchumi na kuchangia fursa mpya za maendeleo, maonyesho hayo ya mwaka huu yanajumuisha makongamano, maonyesho na ushirikiano wa kibiashara na shughuli za utangazaji bidhaa.
Maonyesho hayo, ambayo yamefanyika mara nne, yamekuwa nyenzo muhimu kwa Mkoa wa Liaoning kutekeleza mradi wake wa miaka mitatu wa kupata mafanikio mapya katika ustawi kamili wa kiuchumi. Pia yanatumika kama jukwaa la hali ya juu la kuunda fursa mpya wa ufunguaji mlango kaskazini mashariki mwa China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma