Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping awatembelea wanakijiji walioathiriwa na mafuriko katika Mkoa wa Heilongjiang, China
HARBIN - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amewatembelea wanakijiji walioathiriwa na mafuriko katika Mji wa Shangzhi ulioko Mkoa wa Heilongjiang, Kaskazini Mashariki mwa China.
Katika Kijiji cha Longwangmiao, Rais Xi aliingia kwenye mashamba kuangalia hali ya athari za mafuriko kwenye mazao ya mpunga. Pia alikagua kazi ya ukarabati wa nyumba na miundombinu iliyoharibika wakati akitembea barabarani.
Akitembelea nyumba za wanavijiji ili kufahamu kuhusu hasara zao na utoaji wa huduma za mahitaji muhimu ya kila siku, Rais Xi amewahimiza kuongeza imani na ujasiri wao ili kuyashinda matatizo. Ameelezea imani na matumaini yake kwamba katika muda mfupi ujao wataweza kuanza tena kazi na maisha ya kawaida, na kwamba maisha yao yataendelea kuimarika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma