Lugha Nyingine
Maonyesho ya bidhaa?na?biashara yafunguliwa huko Xinjiang yakilenga kukuza biashara (2)
URUMQI - Maonyesho ya China ya Bidhaa na Biashara kati ya Ulaya na Asia, Eurasia (EACT Expo) 2023 yamefunguliwa Alhamisi huko Urumqi, Mji Mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, Kaskazini-Magharibi mwa China, yakilenga kukuza biashara.
"Kueneza Moyo wa Njia ya Hariri, Kuimarisha Ushirikiano kati ya Ulaya na Asia" ndiyo kaulimbiu ya maonyesho hayo ya mwaka huu, ambayo yanajumuisha eneo la maonyesho lenye ukubwa wa mita za mraba 70,000.
Mashirika saba ya kimataifa yanashiriki katika maonyesho hayo ambayo pia yamevutia zaidi ya kampuni 1,300 kutoka nchi na kanda 40, ikiwa ni pamoja na kampuni 25 kati ya kampuni 500 bora duniani, kwa mujibu wa waandaaji wa shughuli hiyo.
Jumla ya shughuli 33 za kutangaza biashara na uwekezaji zitafanyika wakati wa maonyesho hayo ya siku tano. Pembezoni mwa maonyesho hayo, pia kutakuwa na makongamano yenye mada kama vile ushirikiano wa kiuchumi wa kikanda.
Maonyesho ya China ya Bidhaa na Biashara kati ya Ulaya na Asia yamefanyika mara tatu tangu Mwaka 2015, yakivutia kampuni zaidi ya 3,700 kutoka nchi na maeneo 47.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma