Lugha Nyingine
Sekta ya magari ya China yashuhudia ukuaji wenye sifa ya juu (7)
Mfanyakazi akiwa kazini katika kampuni ya magari mapya ya nishati mpya katika kiwanda cha Chery mjini Wuhu, Mkoa wa Anhui nchini China, Oktoba 12, 2022. (Xinhua/Zhou Mu) |
Gari la milioni tano la nishati mpya (NEV) la kampuni inayoongoza ya China ya magari ya nishati mpya ya BYD lilitolewa siku ya jumatano kutoka kiwandani, na kuifanya China kuwa nchi inayoongoza duniani kwa uzalishaji na uuzaji wa magari duniani kwa miaka 14 mfululizo, na uzalishaji na mauzo ya magari mapya ya nishati (NEVs) yamekuwa ya kwanza katika soko la kimataifa kwa miaka minane mfululizo.
Mauzo ya magari ya China yaliongezeka kwa karibu magari milioni 1.07 katika robo ya kwanza ya 2023, takwimu kutoka kwa Idara kuu ya Forodha ya China, zinaonesha kuwa China imekuwa muuzaji mkubwa zaidi wa magari katika kipindi hicho na kuipita Japan.
Magari ya nishati mpya yamekuwa yakivutia zaidi wateja wa China. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Shirikisho la Viwanda vya Magari vya China, viwanda vya magari vya China vilisafirisha nje magari laki 4.57 kuanzia Januari hadi Mei mwaka huu, likiwa ni ongezeko la mara 1.6 katika kipindi kama hicho mwaka jana.
Tangu 2020, wafanyabiashara wa magari ya umeme nchini China wameanza kuingia katika soko kuu la magari nje ya nchi na kuwa washindani zaidi wakitegemea teknolojia na mikakati inayolenga soko.
Habari ya Picha: Mandhari Nzuri ya Mbuga ya Milimani huko Yunnan, China
Wakulima washughulikia kuvuna mazao ya mbegu za mayungiyungi huko Wilaya ya Quannan, Mkoa wa Jiangxi
Panda "Ruyi" na "Dingding" washerehekea siku ya kuzaliwa huko Moscow
Safari isiyoweza kusahaulika ya mcheza dansi wa Russia katika Mkoa wa Xinjiang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma