Lugha Nyingine
AfDB: Ukuaji wa uchumi wa Afrika Mashariki utaongezeka hadi kufikia asilimia 5.1 mwaka huu
Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB imesema ukuaji wa uchumi wa Afrika Mashariki unakadiriwa kuongezeka hadi kufikia asilimia 5.1 mwaka huu kutoka asilimia 4.4 ya mwaka jana.
Kwa mujibu wa ripoti ya "Mtazamo wa Uchumi wa Afrika Mashariki mwaka 2023" inayoonesha tathmini ya AfDB kuhusu hali ya uchumi ya kanda hiyo, makadirio ya muda wa kati na hatari kwa mustakabali wa ukuaji na uimarishaji wa uchumi katika nchi za Afrika Mashariki zilizochaguliwa utachochewa na kuimarika kwa sekta ya huduma na mauzo kwa nje.
Ripoti hiyo pia imechunguza hali ya ukuaji wa kanda hiyo, vichocheo vyake na mustakabali pamoja na athari kwa maendeleo ya uchumi na jamii, ikionesha kuwa kanda ya Afrika Mashariki inakabiliwa na hatari za kushuka kwa uchumi za ndani na nje ambazo zinaweza kuathiri ukuaji chanya.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma