Lugha Nyingine
Malawi kuongeza mauzo ya bidhaa zake kwa China
Waziri wa biashara na viwanda wa Malawi Bw. Simplex Chithyola Bandaafter amesema serikali ya Malawi inatarajia kuongeza mauzo ya bidhaa zake kwa China, ili kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya pande mbili.
Amesema Malawi imeidhinisha kuuza maharagwe ya soya, maharagwe makavu na chai kwa China, na pande hizo mbili zinahimiza kuidhinisha bidhaa nyingine za kilimo ikiwemo pilipili na ufuta.
Chini ya mfumo wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC, China imesamehe ushuru kwa bidhaa nyingi zinazouzwa China kutoka Malawi kuanzia mwaka 2008, na sasa bidhaa zaidi ya asilimia 97 za Malawi zinaweza kuuzwa China bila ya ushuru.
Mwezi Juni Malawi ilifungua ubalozi mdogo mjini Changsha, mkoani Hunan, ili kuhakikisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara na China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma