Lugha Nyingine
Volkswagen kuimarisha ushirikiano na washirika wa China kwenye soko la magari yanayotumia umeme
Gari la Kampuni ya Volkswagen na SAIC, Modeli ya ID.6 X likionyeshwa kwenye Maonyesho ya 20 ya Shanghai ya Viwanda vya Magari vya Kimataifa huko Shanghai, Mashariki mwa China, Aprili 24, 2023. (Xinhua/Fang Zhe)
FRANKFURT - Kundi la kampuni za Volkswagen, kampuni inayoongoza kwa kuunda magari nchini Ujerumani, imesema Jumatano kwamba inalenga kuimarisha ushirikiano na washirika wa ndani wa China ili kutumia soko linalokua la magari yanayotumia nishati ya umeme.
Kampuni hiyo inachukua asilimia 4.99 ya hisa katika kampuni inayoanza ya kuunda magari yanayotumia nishati ya umeme ya XPeng ya China zenye thamani ya karibu dola milioni 700 za Kimarekani kwa njia ya kuongeza mtaji.
Sambamba na hilo, chapa ya Audi ya kundi hilo la Kampuni za Volkswagen imetia saini mkataba wa kimkakati na mshirika wake wa ubia wa China SAIC ili kupanua zaidi ushirikiano wao uliopo.
"Lengo ni kutumia fursa kwa haraka katika sehemu mpya za wateja na soko, na hivyo kutumia kwa utaratibu uwezekano wa soko la China linalokua kwa kasi la kutumia wa vyombo vya usafiri vinavyotumia umeme," kundi hilo la kampuni limesema katika taarifa kwa vyombo vya habari.
Picha hii iliyopigwa Julai 4 2022 ikionyesha karakana ya kiwanda cha kuunda magari cha Kampuni ya Volkswagen Anhui MEB (Modular Electric Drive Matrix) inayoendelea kujengwa katika Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China. (Xinhua)
Kuongezeka kwa ushirikiano nchini China kunaendana na mkakati wa kundi hilo la kampuni wa "nchini China kwa China", imeongeza taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa makubaliano ya mfumo wa kiteknolojia na XPeng, modeli mbili za magari yanayotumia nishati ya umeme zenye chapa ya Volkswagen kwa sehemu ya ukubwa wa kati zitazinduliwa Mwaka 2026 nchini China. Audi, kwa upande mwingine, pia itaharakisha juhudi zake "kupanua uwanja wa magari yanayotumia umeme yaliyounganishwa kikamilifu yaliyo kwenye ofa kwa haraka na kwa ufanisi."
Akizungumzia hatua hiyo, Ralf Brandstaetter, Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu (Mkurugenzi Mtendaji) wa Kundi la Kampuni za Volkswagen nchini China, amesema kuwa "Ushirikiano wa nchini China ni nyenzo muhimu ya kujenga mkakati wa Kundi la Volkswagen wa 'nchini China kwa China'.
Kundi hilo la Kampuni za Volkswagen limeamua kuongeza juhudi zake nchini China wakati ambapo mauzo yake yalipungua kidogo kwa asilimia 2 katika nchi hiyo ya Asia katika nusu ya kwanza ya Mwaka 2023.
Gari la Audi Modeli ya e-tron GT likionyeshwa kwenye Maonyesho ya 20 ya Shanghai ya Viwanda vya Magari vya Kimataifa huko Shanghai, Mashariki mwa China, Aprili 18, 2023. (Xinhua/Wang Xiang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma