Lugha Nyingine
IMF yakadiria ukuaji wa uchumi?duniani kupungua hadi asilimia 3?Mwaka 2023 na 2024
Picha ya kumbukumbu iliyopigwa Aprili 6, 2021 ikionyesha mandhari ya nje ya makao makuu ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mjini Washington, D.C., Marekani. (Picha na Ting Shen/Xinhua)
NEW YORK - Ukuaji wa uchumi duniani unatarajiwa kushuka kutoka wastani wa asilimia 3.5 Mwaka 2022 hadi asilimia 3.0 Mwaka 2023 na 2024, na ukuaji wa uchumi wa China hautabadilika katika kiwango cha asilimia 5.2 Mwaka 2023 na asilimia 4.5 Mwaka 2024, limesema Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) siku ya Jumanne.
IMF imesema katika ripoti yake mpya ya Mtazamo wa Uchumi wa Dunia kwamba, "ingawa makadirio hayo ya Mwaka 2023 ni ya juu zaidi kuliko ilivyokadiriwa katika Mtazamo wa Uchumi wa Dunia wa Aprili 2023, bado ni dhaifu kwa kulinganishwa na viwango vya kihistoria, kupanda kwa viwango vya sera za benki kuu katika kupambana na mfumuko wa bei kunaendelea kuathiri shughuli za kiuchumi."
IMF imesema, mfumuko wa bei wa kimataifa unatarajiwa kushuka kutoka asilimia 8.7 Mwaka 2022 hadi asilimia 6.8 Mwaka 2023 na asilimia 5.2 Mwaka 2024. Mfumuko wa bei wa msingi unatarajiwa kupungua hatua kwa hatua, na makadirio ya mfumuko wa bei Mwaka 2024 yamerekebishwa kwenda juu.
Ripoti hiyo imesema, kwa nchi zilizoendelea kiuchumi, ukuaji wa uchumi unatarajiwa kushuka kwa kiwango kikubwa Mwaka 2023 -- kutoka asilimia 2.7 Mwaka 2022 hadi asilimia 1.5 Mwaka 2023.
Takriban asilimia 93 ya nchi zilizoendelea kiuchumi zinakadiriwa kuwa na ukuaji mdogo wa uchumi Mwaka 2023, na ukuaji wa Mwaka 2024 kati ya nchi hizo unatarajiwa kubaki katika asilimia 1.4, imesema ripoti hiyo.
Nchini Marekani, ukuaji wa uchumi unatarajiwa kupungua kutoka asilimia 2.1 Mwaka 2022 hadi asilimia 1.8 Mwaka 2023 na zaidi hadi asilimia 1.0 Mwaka 2024.
Ukuaji wa uchumi katika masoko yanayoibukia na nchi zinazoendelea kiuchumi unatarajiwa kuongezeka huku ukuaji wa mwaka hadi mwaka ukiongezeka kutoka asilimia 3.1 Mwaka 2022 hadi asilimia 4.1 mwaka huu na ujao.
Picha: Alama kama mishipa kwenye kando ya Mto Huanghe huko Henan, China
Onyesho la mitindo ya mavazi lafanyika kando ya Tamasha la 6 la Kimataifa la Dansi la China Xinjiang
Zaidi ya wasanii 1,000 waleta sanaa ya kale kwenye tamasha la dansi la Xinjiang
Sarakasi za kijadi zang'ara katika Mji wa Wuqiao, mkoani Hubei, Kaskazini mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma