Lugha Nyingine
Kuku wa kisasa wanaozalishwa na China wavunja ukiritimba wa soko wa nchi zilizoendelea wa miongo mingi
Maafisa wa forodha wakikagua vifaranga walio tayari kusafirishwa kwenye forodha ya Pinggu hapa Beijing, China tarehe 16, Juni, 2023. (Picha kwa hisani ya Kampuni ya Kuku ya Yukou)
Asubuhi ya tarehe 16, Juni, 2023, ndege ya safari TC403 ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ilitua kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere baada ya safari ya masaa 11. Huenda abiria wa ndege hiyo hawakutambua kuwa chini ya ndege hiyo kulikuwa na kundi la “wageni” maalumu – vifaranga 16,500 kutoka Beijing.
Vifaranga hao ni pamoja na kuku wa kuzaliana 15,500 wa “Jinghong 1” wenye uwezo mkubwa wa kutaga mayai, na wengine 1,000 wa nyama aina ya “Wode 188” wenye manyoya meupe, ambao wote wamezaliana chini ya utaalam wa Kampuni ya Kuku ya Yukou ya Beijing Huadu. Hii ni mara ya kwanza kwa China kuuza nchi za nje kuku ambao wamezaliana kwa utaalam wa ndani ya nchi hiyo yenyewe.
Wakati wakifika Tanzania, kuku hao walifikia kiwango cha kuishi kwa asilimia 98.92. Zaidi, hata baada ya kufika kwenye shamba la kuku huko, kiwango cha kuishi kwao bado kilikuwa juu ya asilimia 97, na kuku hao wamekuwa wakiendelea kuishi katika hali nzuri ya afya, kwa mujibu wa Fan Shijie, mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha utafiti na uzalishaji wa Kuku cha Yukou, ambaye alisimamia kazi hiyo ya uuzaji nchi za nje kwa mara ya kwanza kuwahi kutokea.
Uuzaji huo nchi za nje wa kuku wa nyama wa “Wode 188” waliozaliana kwa utaalam wa nchini China pia una umuhimu mkubwa kwa soko la kimataifa, kwa sababu hii ni mara ya kwanza kwa kampuni ya China “kuvunja ukiritimba” wa soko wa muda mrefu ulioshikwa na kampuni za Ulaya na Marekani.
Uuzaji huo wa mafanikio wa mwezi wa Juni ni matokeo ya mchanganyiko wa mambo mbalimbali, ikiwemo wito wa nchi hiyo wa kustawisha tena tasnia ya mbegu ya ndani kama sehemu ya kuadhimisha kutimia miaka 10 tangu kutolewa pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na pia urafiki wa kina kati ya China na Tanzania, Fan amesema.
Maafisa wa forodha wakikagua vifaranga walio tayari kusafirishwa kwenye forodha ya Pinggu hapa Beijing, China tarehe 16, Juni, 2023. (Picha kwa hisani ya Kampuni ya Kuku ya Yukou)
Zaidi ya wasanii 1,000 waleta sanaa ya kale kwenye tamasha la dansi la Xinjiang
Sarakasi za kijadi zang'ara katika Mji wa Wuqiao, mkoani Hubei, Kaskazini mwa China
Mji wa Qingzhen wa China: Mandhari Nzuri ya Milima na Maziwa Yaonekana wazi
Katika Picha: Sao Tome na Principe yaadhimisha miaka 48 tangu kupata uhuru wake
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma