Lugha Nyingine
China kutoa hatua zaidi za kuimarisha?uchumi wa kibinafsi
Mfanyakazi akiuza wigi kwa masoko ya ng'ambo kupitia jukwaa la biashara ya mtandaoni kwenye kampuni ya wigi huko Shaoyang, Mkoa wa Hunan, Katikati mwa China, Mei 25, 2023. (Xinhua/Xue Yuge) |
BEIJING - Maafisa wa Serikali ya China siku ya Alhamisi wameahidi kuwa China itafanya juhudi zaidi za kuimarisha uchumi wa kibinafsi, na hatua zaidi zitatolewa hivi karibuni.
Kauli zao zinakuja baada ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Baraza la Serikali ya China kutoa mwongozo siku ya Jumatano juu ya kuhimiza ukuaji wa uchumi wa kibinafsi.
"Uchumi wa kibinafsi kwa muda mrefu umekuwa na mchango mkubwa katika kuleta utulivu, kukuza uvumbuzi, kuongeza ajira na kuboresha maisha ya watu," Li Chunlin, Naibu Mkuu wa Kamati ya Kitaifa ya Maendeleo na Mageuzi ya Kina ya China, amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari.
"Ili kuhakikisha utekelezaji kamili wa mwongozo huo, kamati itashirikiana na pande husika kuanzisha sera na hatua zinazounga mkono siku za usoni," amesema Li.
Amesema, kama sehemu ya hatua zinazounga mkono, kamati hiyo itachapisha waraka hivi karibuni juu ya kuhimiza uwekezaji wa kibinafsi ili kuhamasisha sekta kikamilifu.
Ameeleza kuwa kamati itaendelea kufanya makongamano na wajasiriamali binafsi mara kwa mara ili kuwasaidia kutatua matatizo na kuzingatia mapendekezo yao.
An Lijia, Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda na Biashara la China, ameahidi juhudi za kuweka mazingira mazuri ya kijamii ya kukuza uchumi wa kibinafsi.
"Tutaongeza utangazaji kwa umma kuhusu wajasiriamali binafsi bora na kueneza moyo wao wa ujasiriamali. Wakati huo huo, tutashirikiana na idara husika ili kukabiliana na uvumi mbaya na kashfa dhidi ya kampuni za kibinafsi," An amesema.
Nchini China, zaidi ya asilimia 90 ya kampuni za binafsi ni ndogo na za kati (SMEs), na zaidi ya asilimia 90 ya SMEs ni kampuni binafsi.
Sekta ya kibinafsi inachangia takriban asilimia 50 ya mapato ya kodi ya China, asilimia 60 ya Pato la Taifa, asilimia 70 ya uvumbuzi wake wa kiteknolojia, na inachangia asilimia 80 ya ajira zote za mijini.
Sarakasi za kijadi zang'ara katika Mji wa Wuqiao, mkoani Hubei, Kaskazini mwa China
Mji wa Qingzhen wa China: Mandhari Nzuri ya Milima na Maziwa Yaonekana wazi
Katika Picha: Sao Tome na Principe yaadhimisha miaka 48 tangu kupata uhuru wake
Picha: Mandhari Nzuri ya eneo la msitu wa mawe wa Zecha huko Luqu, Kaskazini Magharibi mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma