Lugha Nyingine
Uchumi wa China washuhudia hali ya kuimarika katika nusu ya kwanza ya mwaka huu wakati uchumi wa dunia unashuka (4)
Picha ikimwonyesha Fu Linghui, msemaji wa Idara ya Taifa ya Takwimu ya China, akihudhuria Mazungumzo ya Kiuchumi ya China mjini Beijing, China. (Xinhua/Jin Liangkuai) |
BEIJING –Mwelekeo wa uchumi wa China katika nusu ya kwanza (H1) ya Mwaka 2023 umeonyesha dalili za kuimarika wakati ambapo unakabiliana na changamoto mbalimbali, wazungumzaji waalikwa wameyasema hayo kwenye Mazungumzo ya Kiuchumi ya China, ambayo ni jukwaa la mazungumzo linaloandaliwa na Shirika la Habari la China, Xinhua.
Takwimu zilizotolewa na Idara ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) Jumatatu zimeonyesha kuwa, pato la Taifa la China (GDP) lilikua kwa asilimia 5.5 katika nusu ya kwanza ya Mwaka 2023 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huo.
Msemaji wa NBS Fu Linghui amesema ukuaji wa uchumi wa China umeongezeka kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na mwaka jana, hali ambayo ni ya kustaajabisha sana kutokana na kusuasua na kushuka kwa uchumi wa Dunia.
"Katika kipindi cha Januari hadi Juni, usambazaji wa bidhaa za kilimo na viwanda uliendelea kuongezeka, tasnia ya huduma na matumizi ilikua kwa kasi, na maendeleo yenye ubora wa hali ya juu yalipata maendeleo thabiti," amesema.
Tangu Aprili, mashirika na taasisi za kimataifa, kama vile Umoja wa Mataifa, Benki ya Dunia, na Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD), yameongeza makadirio yao ya ukuaji wa uchumi wa China mwaka huu, na kuonyesha imani ya Dunia katika matarajio ya maendeleo ya uchumi wa China.
"Ukikabiliwa na ukuaji duni wa uchumi wa Dunia na kudorora kwa biashara ya kimataifa, ukuaji wa uchumi wa China katika nusu ya kwanza ya mwaka ulishuhudia ongezeko la mchango wa mahitaji ya ndani katika manunuzi kwa Pato la Taifa ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana na mwaka mzima wa 2022," amesema Li Hui, afisa mwandamizi wa Kamati ya Kitaifa ya Kuendeleza Mageuzi ya Kina ya China.
Liu Yuanchun, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Fedha na Uchumi cha Shanghai, amesema kuwa mwelekeo wa uchumi wa China katika nusu ya kwanza ya mwaka huu bila shaka unawakilisha mfano wa ukuaji wa kasi kati ya nchi zenye uchumi mkubwa.
"Ufufukaji wa uchumi katika kipindi cha baada ya janga (la UVIKO-19) ni tofauti na ufufukaji wa kawaida na kwa vipindi kila baada ya muda fulani ambako tumekuwa tukishuhudia hapo awali," amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma