Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping aelezea sera ya China kuhusu nchi za visiwa vya Pasifiki
Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Visiwa vya Solomon Manasseh Sogavare aliye ziarani nchini China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Julai 10, 2023. (Xinhua/Zhang Ling)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Waziri Mkuu wa Visiwa vya Solomon Manasseh Sogavare ambaye yuko ziarani nchini China hapa Beijing, Jumatatu alasiri.
Katika mazungumzo yaliyofanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma, Rais Xi amesema kwa vile China na nchi za visiwa vya Pasifiki ni nchi zinazoendelea, zinapaswa kuimarisha kusaidiana na kuungana mkono chini ya mfumo wa ushirikiano wa Kusini na Kusini.
Ameeleza kuwa China inaheshimu kikamilifu mamlaka ya nchi na uhuru wa nchi za visiwa vya Pasifiki, na inashikilia usawa wa nchi zote, kubwa au ndogo.
Amesema China inaheshimu kikamilifu matakwa ya nchi za visiwa vya Pasifiki na inafuata mashauriano ya kina, mchango wa pamoja, manufaa ya pamoja na matokeo yenye faida kwa pande zote.
“China inaheshimu kikamilifu mila za kitamaduni za nchi za visiwa vya Pasifiki, na inatilia maanani maelewano kati ya uanuai wa tamaduni na kuchangia uzuri wa pamoja wa tamaduni mbalimbali” amesema Rais Xi.
Ameongeza kuwa, China inaheshimu kikamilifu umoja na kujitegemea kwa nchi za visiwa vya Pasifiki, na inaziunga mkono katika kutekeleza Mkakati wa Mwaka 2050 wa Bara la Pasifiki la Bluu, kuchangia katika ujenzi wa Pasifiki ya Bluu yenye amani, maelewano, salama, jumuishi na yenye mafanikio.
Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Visiwa vya Solomon Manasseh Sogavare aliye ziarani nchini China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Julai 10, 2023. (Xinhua/Zhang Ling)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma