Lugha Nyingine
Mazoezi ya operesheni maalum ya skauti polisi wenye silaha yaleta hisia ya "kasi na shauku"?Mjini Tianjin, China
Hivi majuzi, Kikosi cha Pikipiki cha Jeshi la Askari Polisi wenye Silaha wa Mji wa Tianjin nchini China kililenga kufanya mazoezi ya operesheni maalum kwa uhalisia na kuwapanga askari wa kikosi cha upelelezi kutekeleza mafunzo maalum ya kuendesha pikipiki.
"Ni kwa kuigiza mazingira halisi ya vita na kuwa karibu na mahitaji ya mapigano halisi wakati wa mafunzo ndipo tunaweza kuboresha uwezo wa madereva wa kuendana na hali ya vita na kuweza kuwa hai, na kuhakikisha kwamba wakati vita vinapokuja, tunaweza kuchukua fursa hiyo kwa muda mfupi zaidi." kiongozi wa kikosi Zhu Qiguang amesema.
Kwa mujibu wa mahitaji ya mpango mpya wa mafunzo ya kijeshi, kikosi hicho kimeweka kwa uangalifu masomo ya mafunzo chini ya hali halisi ya mapigano kama vile kuinama, namna ya kutembea kwa ukakamavu, kupita vizuizi, kuendesha vyombo vya moto na kupiga risasi. (Picha na Meng Shaoyang, Cao Taike, Cai Zhicun, Wang Liang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma